KENYA YAKUBALI SHISHA INACHANGANYWA NA COCAINE, TANZANIA JE?
Wakati dunia nzima leo ikiadhimisha Siku ya Tumbaku Duniani, kwa upande wa serikali ya Tanzania iliarifu kuwa ipo katika hatua za mwisho za uchunguzi kuhusu shisha na itatoa tamko rasmi juu ya matumizi ya shisha katika sehemu za starehe na mikusanyiko ya watu; hayo ni kwa mujibu wa hotuba ya Aprili 30, 2016 bungeni ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.
Lakini nchini Kenya imekuwa tofauti baada ya Wizara ya Afya nchini humo kumaliza uchunguzi wake na kusema imebaini asilimia 80 yaShisha inayovutwa nchini humo ina chembechembe za Madawa ya Kulevya aina ya Cocaine.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo kupitia mtandao wa Twitter, inasema katika kila kipimo cha shisha kati ya vitano vilivyojaribiwa waligundua kuwepo kwa chembechembe za dawa ya kulevya aina ya Cocaine licha ya kuwepo kwa madawa mengine pia.
Hata hivyo taarifa ya wizara hiyo imeeleza masikitiko yake kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushindwa kuitumia ipasavyo Siku ya Tumbaku Duniani kwa kuonya watu kuhusu madhara yatokanayo na uvutaji wa tumbaku.
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la Kansaya koo, ama mapafu,Matatizo ya Moyo, Fangasi na Kifua Kikuu (TB), Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo), “Nicotine Addiction”, Kupoteza Uwezo za Kujamiiana, Kuchakaa kwa ngozi, Asthma na Allergy nyingine.
Share Post
UnknownWeb Developer
Follow me on:
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
No comments:
Post a Comment