Shirika la kilimo na chakula FAO limetaka uchangishaji wa fedha wa dharura kwa ajili ya kunusuru wakulima wa Ethiopia kuotesha mazao sahambani na kulinda ardhi nchini humo dhidi ya ukosefu wa chakula.
Taarifa ya FAO inasisitiza kuwa ikiwa ni majuma sita kabla ya msimu mkuu wa palizi nchini humo, hali ya upatikanaji wa chakula inatisha, mwitikio wa wito wa changizo dhidi ya janga hauridhishi kutokana na kufikiwa kwa asilimia 15 pekee.
Ikimnukuu mwakilishi wake nchini Ethiopia Amadou Allahoury Diallo, FAO imesema ugawaji wa mbegu ili kusaidia wakulima waoteshe mazao na kuvuna yapaswa kuwa kipaumbele kwa sasa.
Shirika hilo la kilimo na chakula linasema kiasi cha dola milioni 10 kinahitajika katika kipindi cha majuma mawili yajayo ili kuwezesha zoezi la ugawaji mbegu kwa wakulima na kunusuru kaya za Ethiopia dhidi ya njaa.
No comments:
Post a Comment