Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zinazozozana katika mgogoro wa Yemen kuketi kwenye meza ya mazungumzo ya Kuwait kwa nia njema.
Taarifa ya Ban Ki-moon imesema mazungumzo yaliyoanza leo nchini Kuwait chini ya upatanishi wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Ismail Ould Sheikh Ahmad ni hatua muhimu ya kurejesha amani nchini Yemen na kushikamana na usitishaji vita ulioanza tarehe 10 mwezi huu wa Aprili.
Amesema utumiaji mzuri wa fusra hii unaweza kusaidia mchakato wa kurejesha amani na kukomesha vita vya muda mrefu sasa nchini Yemen.
Mazungumzo ya amani ya Yemen yalipangwa kuanza Jumatatu iliyopita nchini Kuwait lakini harakati ya Ansarullah ya Yemen haikuhudhuria mkutano huo baada ya wavamizi wa nchi hiyo wakiongozwa na Saudi Arabia kukiuka makubaliano ya kusitisha vita.
Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na wengine zaidi ya milioni moja kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Waislamu wa Yemen.
No comments:
Post a Comment