Mkufunzi wa timu ya Arsenal Arsene Wenger sasa anasema kuwa uwepo wake katika kilabu hiyo uliisaidia kilabu hiyo kupata mkopo wa ujenzi wa uwanja wa Emirates.
Mashabiki wanatarajiwa kufanya maandamano wiki hii baada ya kukasirishwa na matokeo ya kilabu hiyo msimu huu ambayo yamesababisha timu hiyo kushindwa kushinda taji la ligi.
''Wakati tulipojenga uwanja wa Emirates, benki zilitaka niweke sahihi ya mktaba wa miaka mitano'',alisema Wenger mwenye umri wa miaka 66.
''Wataka kujua ni kilabu ngapi nilikataa wito wao wakati huo''?
Ujenzi wa uwanja wa Emirates uliogharimu pauni milioni 390 ulianza mwaka 2004,mwaka ambapo Wenger alishinda taji lake la mwisho la ligi na kilabu hiyo.
''Benki zilitaka niendelee kuhudumu ili wawe na hakika ya kulipwa fedha zao'',aliongezea Wenger ambaye amekuwa akiisimamia kilabu hiyo tangu mwaka 1996.
No comments:
Post a Comment