Thursday, April 21, 2016

Daesh waua wanawake 250 huko Mosul nchini Iraq


Daesh waua wanawake 250 huko Mosul nchini Iraq
Maafisa wa kikurdi nchini Iraq wametangaza kuwa hivi karibuni magaidi wa kitakfiri wa Daesh wamewaua kinyama wanawake wapatao 250 katika ngome yao kuu huko Mosul kaskazini mwa Iraq. Inasemekana kuwa wanawake hao waliuawa baada ya kukataa kutumiwa na magaidi hao kama watumwa wa ngono.
Gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza limemnukuu Saed Mamouzini, msemaji wa chama cha Wakurdi cha Democratic Party (KDP) akisema kuwa wahanga hao waliamrishwa na matakfiri wa Daesh wakubali kufanya nao zinaa na walipokataa kufanya hivyo waliuawa kinyama, na katika baadhi ya sehemu, wakiwa mbele ya familia zao.
Mji wa Mosul umekuwa chini ya udhibiti wa Daesh tokea mwaka 2014. Matakfiri hao wamekuwa wakiwalazimisha wanawake wanaowakamata mateka kuwa watumwa wao wa ngono na wanapokataa hukabiliwa na hatari ya kifo.
Mwezi Agosti 2014 wanawake na mabinti wapatao 500 wa jamii ya Yazidi walitekwa nyara na magaidi wa Daesh ambapo pia waliwaua kinyama zaidi ya wanaume wao 5000, walipovamia na kuliteka eneo la Sinjar Kaskazini mwa Iraq.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment