Wednesday, April 20, 2016
UMEYA WA JIJI LA TANGA GIZA NENE
Baada ya hayo, April 7, mwaka huu Chama cha Wananchi (CUF) kupitia Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho bara Magdalena Sakaya kumuomba Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuingilia kati mgogoro wa Umeya katika Jiji la Tanga baada ya juhudi mbalimbali za kudai haki kugonga mwamba.
Wakati ombi hilo likisubiriwa, kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Abdul Kambaya ameiambiamtembezi.com katika mahojiano maalumu kuwa hakuna kilichojibiwa na mpaka sasa madiwani watano (5) akiwemo aliye gombea Umeya kupitia CUF wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, nakufanya kuendeleza sintofahamu juu ya mchakato mzima; jambo ambalo Kambaya ameshauri kuwa kama jambo hilo halitapatiwa ufumbuzi wa haraka basi Maendeleo ya Jiji la Tanga yatachelewa na kimsingi wananchi ndio watakaoumia.
Unknown
Web Developer
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment