Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo
kupiga kambi katika Kata ya Miono wilayani Bagamoyo na kuwasaka
wafugaji wanaopiga wakulima.
Waziri
mkuu alitoa agizo hilo alipozungumza na wakazi wa kata hiyo hivi
karibuni alipokwenda kukagua miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani
iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Taarifa
ya Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema diwani wa Miono, Juma Mpwimbwi
akiwasilisha kero zao kwa kiongozi huyo alisema wanakabiliwa na tatizo
la wakulima kupigwa na wafugaji na wakipelekwa kituo cha polisi
hawachukuliwi hatua.
“Wafugaji
wanatupiga lakini wenzetu hawachukuliwi hatua na hata ukienda kushtaki
polisi hawakai kwa sababu wanadai wao wana fedha,” alisema diwani huyo.
Pia,
alisema waliahidiwa barabara ya lami tangu miaka saba iliyopita, lakini
hadi sasa hawana hata kipande kidogo tu cha barabara hiyo.
Mkazi
wa kata hiyo, Shabani Mkwimbi akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake
alisema wana kituo cha polisi na mahakama, lakini utendaji kazi wa
viongozi waliopo unatia shaka.
Alimlalamikia mkuu wa kituo cha polisi na hakimu akidai wafugaji pekee ndiyo wanaoshinda kesi.
Waziri
Mkuu Majaliwa aliwahakikishia wakazi hao kwamba hakuna hata mtu mmoja
ambaye yuko juu ya sheria. Alisema suala la polisi litashughulikiwa na
kamanda wa mkoa.
Majaliwa alisema msimamo wa Serikali ni kuwaona wakulima na wafugaji wanafanya kazi zao kwa uhuru.
“Hakuna
mfugaji anayeruhusiwa kupeleka ng’ombe kwenye mashamba yenye chakula.
Mkuu wa mkoa hili ni agizo, njoo upige kambi hapa na watu wako, na usake
wahusika hadi wabainike. Ni lazima tuwajue ni kina nani wamehusika na
hili,” alisema.
No comments:
Post a Comment