Mwanamuziki
Diamond Platnumz amemuomba msamaha Askofu Gwajima kufuatia kile
kilichodaiwa na askofu huyo kuwa ameimbwa kwenye wimbo wa mtu
anayepotosha haki ili kutetea vyeti feki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo mchana Askofu Gwajima aliandika, “Aliyeniweka kwenye wimbo wa lengo la kupotosha haki ili kusapoti vyeti feki, jiandae, Almasi itageuka maji kesho!”
Kauli
hii ya Askofu Gwajima imekuja ikiwa ni saa chache tu tangu mwanamuziki
Diamond Platnumz alipotoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Acha Nikae
Kimya ambapo ndani ya waliotajwa ni pamoja na Askofu Gwajima. Katika
wimbo huo, Diamond alisema kuwa, ugomvi kati ya Makonda na Gwajima
unachcochewa na dada mmoja kwenye mitandao.
Baada
ya Gwajima kutoka maneno hayo, Diamond amejitokeza na kuandika kwenye
ukurasa wake wa Instagram akifafanua kile alichokiimba kuhusu Gwajima
kuwa hakina lengo baya, huku akimtaka Askofu Gwajima kutomgeuza maji
kesho kanisani kwake, kwani yeye akimpania mtu huwa hatoki
“Yala!
Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu
wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa
nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja
mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na
Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti
mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…” aliandika Diamond na kuongeza;
“Point
yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara
zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa
chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada
mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea
hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭 Chonde chonde
mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua
ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka
mzima😁"
No comments:
Post a Comment