Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja
azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo MONUSCO nchini Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kupunguza idadi ya askari wake.
MONUSCO imeongezewa muda hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani.
Kwa mujibu wa umoja wa mataifa azimio
hilo limegusia suala muhimu lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza
idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa hadi askari 16,215.
Azimio limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa António Guterres kufanya tathmini ya majukumu ya MONUSCO kwa
wakati huu kuona iwapo majukumu yote ni muhimu.
Wanachama wa baraza hilo wamemuonya
raisi Joseph Kabila kwamba utawala wake lazima iheshimu mkataba wa
kusirikiana uongozi na upande wa upinzani na kuruhusu uchaguzi muhimu
kufanyika.
Balozi wa uingereza katika baraza la
usalama la umoja wa mataifa Matthew Rycroft, ambaye alikuwa mwenyekiti
wa baraza mwezi huu ameeleza kuwa ukosefu wa usalama na mvutano
umeendelea kushuhudiwa katika kipindi chote nchini DRC.RFI
No comments:
Post a Comment