Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la
Mecklenburg-Vorpommern yalikuwa pigo la kufedhehesha, lakini kwa uhakika
siyo mwisho wa ukansela wa Angela Merkel, au mwanzo wa kubadili
mwelekeo wa kisiasa, anasema Charlotte Potts.
Mwisho wa Ukansela," Ni makofi mangapi amebakiza Merkel," "Pigo kwa
Merekl," hivyo ndivyo baadhi ya vichwa vya habari vilivyopamba magazeti
ya leo nchini Ujerumani. Kwa miezi kadhaa kuwekuwepo na matukio kama
hayo ambayo yameeashiria kuhitimisha ukansela wa Merkel: baada ya kauli
yake iliyozuwa utata ya Tunamudu mwaka mmoja uliyopita na kuchomwa kwa
makaazi ya wakimbizi, baada ya matukio ya kesha wa mwaka mpya mjini
Cologne, ambamo wakimbizi walidaiwa kuwashambulia wanawake kingono,
baada ya mashambulizi ya kigaidi katika miji ya Würzburg na Ansbach,
ambayo yalifanywa na waomba hifadhi. Na licha ya hayo yote Merkel
ameendelea kuwa Kansela. Na bado anaendelea kushikilia msimamo wake
kuhusu wakimbizi.Uchaguzi wa jimbo usitiwe chumvi
Bila shaka matokeo ya uchaguzi jimboni Mecklenburg-Vorpommern ni pigo la fedheha kwa chama cha CDU. Na bila shaka mafanikio ya chama cha AfD ambacho kwa sasa kinawakilishwa katika majimbo tisa kati ya 16 ya Ujerumani, uvipe changamoto vyama vikuu vya siasa vya Ujerumani. Hakukuwa na chama cha kidemokrasia cha upinzani kwa mrengo wa kulia - lakini kuibuka kwa AfD kumewka chama cha namna hiyo. Na bila shaka sera ya Merkel kuhusu wakimbizi ndiyo ya kulaumiwa - Merkel alifanya uamuzi kuhusu sera hiyo mwishoni mwa majira y akiangazi mwaka 2015.
Alikataa kuwafungia milango wakimbizi waliokuwa wamekwama nchini Hungary, na kwa njia hiyo kukitwika mzingo chama chake. Ukweli kwamba uamuzi mzito kama huo unaambatana na matatizo makubwa ni jambo linalijieleza lenyewe. Lakini pia ukweli kwmaba siyo kila mmoja ndani ya CDU ameshawishika haishangazi. Lakini siyo jambo jipya kwamba wanasiasa watafuta umaarufu wanajribu kuziba ombwe la kisiasa linalosababishwa na vyama vya siasa za mrengo wa kulia wa wastani.
Historia inaonyesha ni jimbo lisilotabirika
Lakini matokeo ya uchagui huu wa jimbo hayapaswi kutiliwa chumvu. Tunazungumzia uchaguzi wa kieneo katika jimbo ambalo mara kadhaa limekuwa likipiga kura za upinzani. Tangu mwaka 2006 chama cha itikadi kali za mrengo wa kulia cha NPD kimekuwa na uwakilishi katika bunge la jimbo hilo. Ni jimbo ambalo kwa kwa miaka kadhaa limekuwa nyumbani kwa siasa kali, ambako siasa kali za mrego wa kulia kama zilivyo za kusohoto, zimekuwa imara. Na ambamo chama cha CDU hata katika uchaguzi wa mwisho miaka mitano iliyopita - muda mrefu kabla ya mgogoro wa wakimbizi, kililishinda zaidi asilimia 20 tu.
Ingekuwa busara zaidi kuhiji na kusema kwamba chama cha CDU kimepoteza tu asilimia nne ya kura katika kipindi9 cha miaka mitano, kipindi ambacmo mambo mengi yamebadilika jimboni humo. Mecklenburg-Vorpommern ni jimbo ambalo halitoi mchango wowote kiuchumi kwa taifa. Likiwa na wapigakura milioni 1.3 ambao ni chini ya asilimia 60 yake ndiyo walishirki uchaguzi huo. Na matokeo ya uchaguzi huo yameamua kuubakiza muungano mkuu. Watu 800,000 tu hawamui hatma ya ukansela.
Tatizo si Merkel
Tatizo halisi la CDU jimboni Mecklenburg-Vorpommern haliko kwa Merkel, bali kwa mgombea wa CDU asie na umaarufu Lorenz Caffier. Kampeini ilionyesha kuwa hakuwa na jipya alilokuja nalo tofauti na AfD. Caffier alijitanabahisha kama mgombea wa usimamizi wa sheria, akitetea upigaji marufuku wa vazi la Burqa. Ni jambo linalotia wasiwasi iwapo kweli wakaazi wa Mecklenburg wanalo tatizo na vazi hilo lilalofunika mwili mzima. Ni wakimbizi 200,000 tu waliopelekewa jimboni humo wakati wa mgawanyo wa wakimbizi katika majimbo na mapaka wakimbizi wengi wamekwisha ondoka huko, hivyo msimamo wa Caffier haukuwa na msaada wowote.
Licha ya hayo CDU na Kansela Merkel wanapaswa kuangalia uchaguzi huo kama wito: siyo kwa ajili ya kubadili meuelekeo wa sera yake bali kuweka ukweli bayana: kwamba katika mwaka wa 2016 wakimbizi wachache sana wameingia Ujerumani, na kwamba wakimbizi wote walioingia awali wamesajaliwa na kupatiwa makazi. Na kwamba wanawasiana vizuri kuhakikisha matatizo yaliokuwepo yanashughulikiwa, kuikamilisha makubaliano na uturuki, kwa sababu ukweli hauko wazi kama AfD inavyojaribu kuuonyesha. Wapugakura wangependa utafutaji kidogo wa umaruf na ukweli zaidi.
No comments:
Post a Comment