Tuesday, March 29, 2016

FREEMAN MBOWE: CCM WAJIPANGE UCHAGUZI UJAO


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa, na kuongeza kuwa matokeo hayo yawe chachu ya kufanya vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.

Mbowe ameeleza kuwa uchaguzi sio tukio, bali mchakato, hivyo kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasa ya urais, watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi.

Mbowe amesema hayo Masaki jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vyema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajili yake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,” amesema Mbowe.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment