Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa wanachunguza madai ''yanayosumbua kwa kiwango kikubwa'' kuhusu unyanyasaji unaotekelezwa na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.
Mwaka uliopita kuna madai 69 ya ubakaji wa watoto pamoja na makosa mengine ya unyanyasaji wa kingono kutoka kwa vikosi 10 vya ujumbe huo.
Kundi moja la utetezi linasema kuwa limepitisha ripoti mpya kwa Umoja wa Mataifa kwamba mwanajeshi mmoja aliwalazimisha wasichana wanne kufanya ngono na mbwa.
Umoja huo umesema kuwa unaangazia idadi kamili ya madai hayo.
Ripoti mpya za unyanyasaji zilitolewa na kundi la kampeni la Code Blue linalosimamiwa na kundi la utetezi la Aids Free World.
Kundi hilo linasema kuwa unyanyasaji huo uliripotiwa kufanywa kati ya mwaka 2013 na wiki hii.
Linasema kuwa madai hayo ya kufanya ngono na wanyama yaliowasilishwa mwaka 2014,yalihusisha kamanda mmoja wa vikosi vya Ufaransa.
Wasichana hao ambao mmoja wao alifariki kutokana na ugonjwa usiojulikana walilipwa faranga 5,000 fedha za Jamhuri ya Afrika ya kati.
No comments:
Post a Comment