Rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni amelazimika kufanya ziara ya ghafla katika eneo la Rwenzori kwenye mpaka wa Uganda na Congo, ambako hali ya wasiwasi inaendelea kuongezeka, vyombo vya usalama vilitoa hesabu ya watu 33 kuuawa hadi sasa kutokana na makabiliano kati ya raia na polisi.
Museveni ametembelea eneo hilo, huku nyumba zikiwa tupu, watu wakitoroka makwao wakitafuta mahali salama licha ya mkuu wa Polisi wa Uganda Jenerali Kaye Kayihura kuamua kukita kambi katika eneo hilo ili kujaribu kumaliza hali ya uhasama kati ya raia na Polisi hao.
Hii ni wiki ya tatu sasa idadi ya watu wanaouwawa kutoka na uhasama kati ya raia na Polisi inaendelea kuongezeka kutokana na ghasia hizo, uhasama huu ulianza pale Polisi walipouwa vijana saba waliokuwa wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku Polisi wakikanusha kwamba ghasa hizo ni za kijamii na sio vurugu za kisiasa.
No comments:
Post a Comment