Thursday, March 31, 2016

Dola milioni 105 zahitajika kuokoa maisha kwenye ukame Somalia



Watoto nchini Somalia. Picha ya UN/Tobin Jones
Mashirika ya kibinadamu nchini Somalia yamezindua leo ombi la msaada wa dola milioni 105 kwa minajili ya kuongeza jitihada za usaidizi wa kunusuru maisha na kujenga uthabiti wa zaidi ya watu milioni moja katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame kaskazini mwa nchi. Taarifa kamili na Flora Nducha
(Taarifa ya Flora)
Ukame huo ambao makali yake yameongezwa na hali ya hewa ya El NiƱo, unaathiri maeneo ya majimbo ya Puntland na Somaliland, ambayo tayari yanakumbana na hali ya kibinadamu yenye rundo la changamoto.
Taarifa ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa (OCHA), imesema watu wapatao milioni 1.7, sawa na ailimia 40 ya idadi nzima ya watu milioni 4.6 wanaoishi katika maeneo hayo, wanahitaji usaidizi wa kibinadamu na kuinuliwa kiuchumi.
Tayari, takriban watu laki nne wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
OCHA imesema iwapo usaidizi wa fedha hautapatikana haraka, madhara ya ukame huo yatakuwa makubwa zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa msimu ujao wa mvua umetabiriwa kuwa usio na mvua tosha
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment