Thursday, March 31, 2016

Kashfa ya Nkandla: mahakama ya Katiba yaamuru Zuma kulipa





Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
© REUTERS/Nic Bothma/Pool/File

Alhamisi hii asubuhi, Mahakama ya Katiba imeamuru Rais wa Afrika Kusini kulipa sehemu ya fedha zilizotumiwa kwa ukarabati wa makazi yake binafsi.

Euro milioni kumi na tano ya fedha za umma zilitumiwa kwa kukarabati kwa makazi yake binafsi ya Nkandla. Hili ni pigo kubwa kwa Rais Jacob Zuma.
Huu ni uamzi unaosisimu ambao umesomwa mapema alhamisi hii asubuhi na jaji mkuu wa Mahakama ya Katiba, Mogoeng Mogoeng. Mhakama ya Katiba imenuagiza Rais Jacob Zuma kulipa asilimia "yenye kueleweka" ya gharama za ukarabati wa makazi yake binafsi katika kijiji cha Nkandla.
Lakini jaji amebaini kwamba kwa kukataa kutii amri ya Mpatanishi wa Jamhuri na kulipa, Rais Zuma "alishindwa katika wajibu wake wa kulinda na kutetea Katiba." Kwa maneno mengine, alivunja Katiba ya nchi.
Uamuzi huu ni mzito wenye kwani unatoa nafasi kwa uwezekano wa utaratibu wakumng'oa mamlakani rais jacob Zuma. Mbali na hilo, chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance, kilipoondoka katika mahakama ya Katiba, kimetangaza kuwa kitaanzisha utaratibu wa kumng'atua madarakani Rais Zuma. Kisha chama cha pili cha upinzani, ambacho kilishawishi vyama vingine kuanzisha mchakato huo, kumetoa wito kwa raia wa Afrika Kusini kuingia mitaani kudai Rais Zuma ajiuzulu.
Sasa Jacob Zuma ana siku 45 kuwa amesha alipa kiwango cha fedha kilioamuliwa na Mahakama ya Katiba.

Makazi ya pili ya Rais Jacob Zuma katika kijiji cha Nkandla, Afrika Kusini
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment