Umoja wa Mataifa umesema kuwa kuendelea mzozo huko Sudan Kusini na raia wa nchi hiyo kukimbilia nchini Sudan kunatia wasiwasi.
Adrian Edwards Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa amesema kuwa ukosefu wa usalama wa chakula na pia ukosefu wa amani huko Sudan Kusini, yote hayo yamesabababisha hadi kufikia mwezi Januari mwaka huu raia elfu 38 wa nchi hiyo kukimbilia Sudan kwa ajili ya hifadhi.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema, mgogoro wa chakula na hali mbaya ya kiuchumi inayosabishwa na mzozo wa ndani khususan katika mkoa wa Upper Nile vinatia wasiwasi mkubwa. Adrian Edwards ameongeza kuwa viongozi wa serikali ya Sudan pia wanahitaji msaada wa fedha na chakula ili kuamiliana na hali hiyo. Sudan Kusini imekumbuwa na mzozo wa ndani tangu mwezi Disemba mwaka 2013. Serikali ya Sudan Kusini na waasi mwezi Agosti mwaka jana walisaini makubaliano ya amani na kusimamisha mapigano, hata hivyo pande hizi zimekiuka makubaliano hayo mara kadhaa.
No comments:
Post a Comment