Tuesday, March 29, 2016

Tibet yarudia ahadi yake ya kupinga kujitenga na China


 
Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulioko kusini magharibi mwa China leo umeadhimisha Siku ya Ukombozi wa Watumwa katika hafla ya kupandisha bendera na ahadi rasmi za kupambana na nia ya kujitenga.
Akihutubia katika hafla hiyo, mkuu wa serikali ya mkoa wa Tibet Losang Jamcan amesema, kundi la Dalai Lama wa 14 halijaacha majaribio yake ya kuigawa China, lakini vitendo hivyo vinapingana na katiba, utaratibu wa nchi, na matakwa ya watu wote wa Tibet, na kamwe havitafanikiwa.
Losang amesema, kundi hilo haliwezi kupinga mafanikio makubwa yaliyopatikana Tibet chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, wala kufifisha maazimio ya Wachina wote, wakiwemo Watibet, ya kulinda umoja wa taifa.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment