Thursday, March 31, 2016

SAMATTA AJIPA MATUMAINI YA KUFUZU AFCON 2017



DAR ES SALAAM


NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta amesema Taifa Stars bado ina nafasi ya kufuzu fainali za Afrika (Afcon) mwakani.

 Samatta anayecheza klabu ya KRC Genk iliyopo Ligi Kuu ya Ubelgiji, alisema amesikia kuhusu timu ya Taifa ya Misri kushinda mchezo wake dhidi ya Nigeria juzi na hivyo kufikisha pointi saba ambazo ndizo Tanzania inaweza kuzifikia ikishinda michezo yake miwili iliyobaki.Samatta

“Nimesikia Misri imeshinda bao 1-0 na sasa wana pointi saba, ukiangalia kwa juujuu unaweza kudhani wameshafuzu, lakini kiuhalisia bado, soka haipo hivyo. “Misri watakuja Dar es Salaam tunaweza kuwafunga kama walivyotufunga kwao (Misri iliifunga Taifa Stars mabao 3-0), pia mechi yetu ya Nigeria tukishinda tutakuwa nasi na pointi saba, tutashindana tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa,” alisema Samatta.

Kwa upande wake Mshauri wa Benchi la Ufundi la Taifa Stars, Abdallah Kibadeni, amesema Stars bado ina nafasi na kwamba matokeo ya Misri yasiwakatishe tamaa mashabiki.


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment