Saturday, April 2, 2016

Kukubaliana Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na uamuzi wa Mahakama ya Katiba



Kukubaliana Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na uamuzi wa Mahakama ya Katiba
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza kuwa, anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Kati ya nchi hiyo dhidi yake.
Rais Zuma alitangaza jana kwamba, anaheshimu uamuzi huo wa mahakama na kwamba, atarejesha katika hazina ya serikali kiasi cha fedha alichotakiwa kukirejesha baada ya kutumia fedha hizo katika mambo yake binafsi. Rais Zuma amesema kuwa, hakukiuka katiba ya nchi kwa makusudi. Rais huyo amesema kuwa, anaomba radhi yeye na kwa niaba ya serikali anawaomba radhi wananchi wa nchi hiyo na anavitaka vyama vyote vya kisiasa kuheshimu katiba.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imemuagiza Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo kuirejeshea serikali fedhai zilizotumika kukarabati makazi yake binafsi, kwenye moja ya kashfa kubwa za ufisadi zilizowahi kuripotiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni. Hatua ya Rais Zuma ya kukarabati makazi yake binafsi kwa bajeti ya serikali, ni jambo ambalo lililipua ghadhabu za wapinzani na kuwakasirisha akthari ya wananchi wa nchi hiyo.
Chama kikuu cha upinzani katika Bunge la Afrika Kusini kimetangaza kuwa, kitatumia kila njia kuhakikisha Zuma anavuliwa madarakani endapo Bunge litazembea kufanya hivyo. Wabunge wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) wametangaza kuwa, wana mpango wa kuwasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo wa kutokuwa na imani na uwezo wa kisiasa wa Rais Zuma.
Jacob Zuma alishika hatamu za uongozi nchini Afrika mwaka 2009 katika hali ambayo, kabla ya kuchukua wadhifa huo, mahakama ilikuwa imemfutia tuhuma 700 za ufisadi wa fedha. Mwaka 2014 alifanikiwa kutetea kiti chake na hivyo kuongoza kwa muhula wa pili. Suala la ufisadi na ubadhirifu wa mali ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika na na viongozi serikali ndio watuhimiwa wakuu. Afrika Kusini nayo kwa mujibu wa asasi za kimataifa ni miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kwa visa vya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma barani Afrika. Hii ni katika hali ambayo, hali mbaya ya uchumi imewafanya wananchi wa nchi hiyo walemewe na mzigo wa mashinikizo ya kifedha na akthari ya wananchi wanalalamikia jambo hilo. Hivi karibuni Rais Jacob Zuma alitangaza nia ya serikali ya kupunguza matumizi ya serikali. Aidha aliahidi katika mkutano wa kiuchumi wa Afrika kupambana na ufisadi wa fedha.
Licha ya kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Afrika Kusini imekuwa ikipiga hatua katika ustawi wa kiuchumi, lakini matatizo ya kisiasa na migogoro kama ya nishati ya umeme na ukame ni mambo ambayo yametoa pigo kwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo. Janga la ukame limepelekea kusimama mwenendo wa ukuaji wa uchumi nchini Afrika Kusini katika miezi mitatu ya mwisho mwa mwaka jana.
Aidha kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia asilimia 25 na kuongezeka idadi ya watu nchini humo walioambukizwa virusi vya ukimwi ni matatizo mengine yanayotajwa na wachambuzi wa mambo kwamba, yameyafanya maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu. Filihali, mazingira magumu ya kiuchumi kwa upande mmoja na suala la viongozi kutumia fedha za umma kwa masuala yao binafsi kwa upande wa pili, ni mambo ambayo yamelipua ghadhabu za vyama na wananchi wa nchi hiyo. Inaonekana kuwa, ahadi ya Rais Zuma ya kurejesha fedha kama alivyotakiwa na mahakama na kusisitiza kufungamana kwake na sheria ni hatua ambayo inalenga kupunguza makali ya mgogoro wa sasa wa nchi hiyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment