Makundi ya waharakati wa kutetea haki za
binadamu yamefanya maandamano katika mji mkuu wa Uingereza London
kulalamikia dhuluma na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya usalama vya
Nigeria dhidi Waislamu wa nchi hiyo.
Mwandishi wa kanali ya televisheni ya Press TV ya Iran
ameripoti kuwa wanaharakati hao wametumia safari ya Rais Muhammadu
Buhari nchini Uingereza kuandamana na kulaani ukandamizaji unaofanywa na
serikali ya rais huyo dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ya magharibi mwa
Afrika. Rais wa Nigeria yuko Uingereza kushiriki mkutano wa kupambana na
ufisadi. Kadhalika wanaharakti hao wameitaka serikali ya Rais Muhammadu
Buhari kumuachia huru msomi wa Kiislamu nchini humo Sheikh Ibrahim
Zakzaky. Wanaharakati hao wa kutetea haki za binadamu wanasema wimbi
hilo la malalamiko ni utangulizi wa kuilazimisha serikali ya Abuja
imwachie huru Sheikh Zakzaky.
Kumekuwepo wasiwasi mkubwa kuhusu ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Nigeria dhidi ya Waislamu hususan wa madhehebu ya Shia nchini humo.
Disemba mwaka jana 2015, jeshi la serikali ya Nigeria lilishambulia kituo cha kidini cha Waislamu hao na kuua mamia miongoni mwao katika mji wa Zaria. Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na wenzake kadhaa pia wangali wanashikiliwa na vyombo vya usalama kwa miezi kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment