Muungano wa
upinzani nchini Kenya CORD unafanya maandamano katika miji mikuu nchini
humo kuwashinikiza maafisa wakuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC)
kujiuzulu.
Viongozi wa muungano huo wamesema maafisa hao hawawezi kuandaa uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na marungu kutawanya maandamano sawa na hayo Jumatatu wiki iliyopita.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu walisema polisi walitumia nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano hayo.
Taarifa kutoka mji wa Mombasa zinasema polisi tayari wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.
Mtu aliyeshuhudia amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema polisi wa kukabiliana na fujo wamekuwa wakishika doria katika barabara za mji huo.
Maduka mengi yamefungwa kutokana na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo na kutokea kwa uporaji.
No comments:
Post a Comment