Kampuni moja huko China imeomba msamaha kwa tangazo la sabuni ambalo limezua utata kwa madai ya ubaguzi wa rangi.
Kampuni hiyo ya Qiaobi , imesema imepinga na kushtumu ubaguzi wa rangi na kuomba radhi kwa tangazo hilo ambalo limezua utata.
Katika tangazo hilo,linamuonyesha mwanamume mweusi akiingiza kichwa chake kwenye mashine ya kufua na baadaye kujitoa akiwa na ngozi nyeupe ya raia wa ki-asia.
Katika taarifa yao ya kuomba msamaha ,kampuni hiyo ya vipodozi ya Shanghai Leishang, imelaumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa kulishtumu tangazo hilo.
Tangazo hilo lilitolewa mara ya kwanza mwezi Machi na kusimamishwa wiki hii kufuatia shinikizo kali.
Katika taarifa hiyo waliwaomba radhi Wafriaka wote na kusema ni matumaini yao kwamba watu na vyombo vya habari hawatazingatia tangazo hilo.
Kampuni hiyo imesema imevifuta viunganishi vyote vya tangazo hilo na kuwataka watu kusitisha usambazaji wake kwenye mitandao.
No comments:
Post a Comment