Rapa,Mwigizaji na mtangazaji Nick Cannon ameweka dola laki moja mezani kwa rapa yoyote nchini Marekani anayeweza kushindana naye kuchana wafanye RAP BATTLE.
Kupitia twitter Nick Cannon amesema ana dola $100,000 kwa rapa atakaye mshinda ataipata, ila pia huyu rapa aweke chini dola laki moja,akishindwa anaipoteza.
Shindano litafanyika kwenye tuzo za 2016 BET Awards mjini Los Angeles mnamo June 25.
Battle rap iliwahi kufanyika kwenye tuzo za BET kati ya Snoop Dogg na Murda Mook kupitia “Gladiator School” na ilikuwa BET Hip Hop Awards mjini Atlanta mwaka 2014
No comments:
Post a Comment