Picha za satellite zilitolewa kwa BBC zinaonyesha kuwa ndege nne za Urusi aina ya helkopta na malori 20 viliteketea moto ndani ya kambi moja ya kijeshi iliyo kati kati mwa Syria wiki iliyopita.
Kampuni moja ya ujasusi ya Marekani, Stratfor, iliyotoa picha hizo, inasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Islamic State walihusika na uharibifu huo.
Islamic state hawajasema kuwa ni wao walihusika lakini taarifa kutoka kwa kundi hilo zinasema kuwa helikopta na malori yaliteketea.
Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa huenda moto ulisambaa kutoka kwa tangi la mafuta ambalo lilipuka. Urusi bado haijazungumzia kisa hicho.
No comments:
Post a Comment