May 19 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amekutana na mabalozi mbalimbali pamoja na katibu mtendaji wa SADC Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo.
Baadhi ya mambo waliyozungumza ni pamoja na mpango wa kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2016 wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Kiwanda hicho kitatumia rasilimali ya gesi asilia na miamba ya matumbawe ‘coral reef’ iliyopo wilayani Kilwa, kitajengwa kwa ubia kati ya Tanzania na nchi za Dernmark, Ujerumani na Pakstani na kitakuwa na uwezo wa kuzalishatani 3800za mbolea kwa siku.
ULIKOSA KILICHOMCHEKESHA
No comments:
Post a Comment