Thursday, May 12, 2016

Rais wa Brazil Dilma Rousself kasimamishwa kazi…


Mtu wangu kama utakuwa karibu na vyombo vya habari vya kimataifa story inayochukua headline sasa hivi ni kuhusu aliyekuwa Rais wa Brazil wa kwanza mwanamke Dilma Rousself kusimamishwa kazi ya urais.
Hatua hiyo imekuja baada ya Bunge la Seneti Brazil kupiga kura kuidhinisha kutokuwa na imani na kiongozi huyo wa Taifa ambapo amesimamishwa kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo likichunguza  tuhuma za rushwa zinazomkabili. 
Masenata 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwa na imani na 22 hawakuunga mkono katika kikao cha zaidi ya saa 20, Makamu wa rais Michel Temer sasa ndio atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment