Takribani mwaka mmoja baada ya kuwa uhamisho ghali uliofeli katika klabu ya Manchester United – Angel Di Maria ameonyesha kwanini Louis van Gaal alikosea kumuuza kwenda PSG.
Kiungo mshambuliaji wa PSG ametengeneza rekodi mpya kwenye ligi ya Ligue 1 kuwa kutoa pasi 18 zilizosababisha magoli kwenye msimu huu.
Di Maria aliwatengenezea magoli Zlatan Ibrahimovic na Lucas Moura katika mchezo wa ushindi wa 4-0 wa PSG dhidi ya Nantes.
Rekodi ya nyuma iliyokuwepo ilikuwa assists 17 ambayo iliwekwa na Marvin Martin wakati akiichezea FC Sochaux msimu wa 2010-11.
Di Maria aliuzwa na Manchester United baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja – PSG walilipa kiasi cha £44 million mnamo mwezi August 2015 ili kupata huduma za kiungo huyo wa Argentina.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari ameshashinda ubingwa wa Ligue 1 na pia anaweza kushinda kombe la Ufaransa ikiwa PSG wataifunga Marseille katika mchezo wa fainali baadae mwezi huu.
No comments:
Post a Comment