Monday, May 16, 2016

AZAM FC ‘WANASHANGAZA’ SANA KATIKA MACHAGUO YAO YA MAKOCHA


IMG-20160513-WA0012
IMG-20160513-WA0012
AZAM FC wanashangaza sana kwa kweli! Ukiniuliza Azam inahitaji nini zaidi? Jibu langu ni kocha bora mwenye uzoefu na mpira wa Afrika. Mfano, Mnigeria, Stephen Keshi ama pengine Mscotland, Bobby Williamson ambaye kwa miaka nane amekuwa na kazi yenye mafanikio katika Afrika Mashariki na Kati.
Sijui lolote kuhusu kocha Mspaniola ambaye ameingia nchini Ijumaa kufanya mazungumzo ya kukinoa kikosi hicho ambacho kwa hakika kitashiriki katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baadae mwaka ujao.
Nilikwisha andika mara kadhaa kuhusu uwezo wa kiufundishaji wa kocha wa sasa Muingereza, Stewart Hall ambaye kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne ataachia kazi. Azam FC imejipotezea muda kwa uamuzi wake wa kumrejesha Hall ili kuchukua nafasi ya Mhindi, Boris Bunjak mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2012/13.
Hall alijiunga kwa mara ya kwanza na Azam FC mwezi Disemba  2010 akitokea Zanzibar alikokuwa akiinoa timu ya Taifa ‘Zanzibar Heroes.’
Kabla yake Azam ilikuwa ilifundishwa na Wabrazil, Neider Santos ambaye alikuwa kocha wa kwanza kuifundisha timu katika Ligi kuu msimu wa 2008/09, kisha akafuata aliyekuwa msaidizi wa Santos, raia mwenzake wa Brazil, Itamor Amourin ambaye alikinusuru kikosi hicho kutoshuka katika msimu wao wa kwanza VPL.
Itamour alikuja kuondolewa kwa kuwa Azam ilihitaji kocha atayewapa mafanikio ya haraka katika VPL ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya CAF. Hall aliamalizia msimu wa 2010/11 na kuisaidia Azam kumaliza nafasi ya tatu katika ligi kuu.
Nafasi hiyo iliwapa tiketi ya kucheza michuano ya CECAFA Kagame Cup kwa mara ya kwanza mwaka 2012. Msimu wa 2011/12 Muingereza huyo akaisaidi Azam kumaliza katika nafasi ya pili katika VPL, kisha kuifanikiwa kufika fainali katika michuano yao ya kwanza za kimataifa (Kagame Cup 2012) mchezo ambao walipoteza 2-0 dhidi ya Yanga SC.
Hall akafukuzwa kazi kwa kile kilichodaiwa kukaidi maagizo ya bosi wake kutomchezesha kiungo mshambulizi, Mrisho Ngassa katika mchezo wa fainali. Ngassa aliibusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati alipofunga goli pekee la Azam akitokea benchi katika pambano la nusu fainali dhidi AS Vita Club ya DR Congo.
Hall aliondolewa kwa sababu zisizo za kimpira na mtu aliyechukua nafasi yake Agosti 2012, Bunjak hakufaa kwa maana tayari Azam ilikuwa imesogea mbele kiuchezaji. Makosa ya kumtimua Hall yaliigarimu sana timu hiyo kwa kuwa wachezaji wa Azam wanampenda sana kocha huyo. Akarudishwa miezi mitatu baadae na kuisaidia tena Azam kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu msimu wa 2012/13.
Katika michuano ya Shirikisho Afrika mwaka 2013 ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwa Azam FC katika michuano ya CAF, Hall alifanikiwa kuisaidia Azam kufika hadi hatua ya 16 bora. Alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na Azam ilionekana inahitaji zaidi taji la ligi kuu.
Miaka mitatu iliyopita wakati Azam ilipozidiwa dakika za mwisho na Yanga katika michezo ya VPL na kushindwa kutwaa ubingwa msimu wa 2012/13 nilishauri kuwa timu hiyo inapaswa kusaka kocha mwenye mbinu zaidi ya Hall ili wapate ubingwa wao wa kwanza wa VPL.
Hall licha ya vikosi vyake kucheza vizuri, mbinu zake katika michezo ya kuamua ubingwa hazijawahi kuwa bora. Hata msimu huu amefanikiwa kupata pointi nne tu katika michezo minne dhidi ya washindani wake wakubwa katika taji, timu za Yanga na Simba.
Hata wakati ule alipoisaidia kumaliza katika nafasi ya pili msimu wa 2011/12 na 2012/13 Hall alishindwa katika mipambano muhimu dhidi ya washindani wake wa ubingwa. Aliondolewa mara baada ya kumalizika kwa michezo ya mzunguko wa kwanza VPL msimu wa 2013/14 na nafasi yake ikaangukia kwa Mcameroon, Joseph Omog ambaye alikuwa mshindi wa kombe la Shirikisho Afrika mwaka mmoja nyuma akiwa na timu ya AFC Leopard ya Congo Brazzaville.
Omog aliipa Azam FC ubingwa wa kwanza wa VPL Mei 2014 huku mbinu zake dhidi ya Yanga na Simba zikiwa ni kusaka matokeo zaidi. Alifukuzwa baada ya Azam kupoteza 3-0 ugenini dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika, Februari 2015.
Hall akarejeshwa mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2014/15. Ameisaidia Azam FC kushinda ubingwa wa kwanza wa Kagame Cup Julai 2015 lakini katika ligi ameendelea kuchemsha. Amekuwa mlalamishi mno kuhusu waamuzi hasa timu yake inaposhindwa kupata matokeo.
Kama unakumbuka baada ya Azam kuchapwa 3-0 na Esperance ya Tunisia na kuondolewa kwa jumla ya magoli 4-2 katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Shirikisho niliandika kuwa Azam inahitaji kocha mpya mwenye mbinu, uzoefu na mpira wa Afrika na nikatolea mfano mshindi wa CAN 2013, Keshi.
Ila wamemleta mtu mpya kabisa na Afrika, kigezo kikubwa ni nchi anayotoka. Naye tutamfahamu kisha tutajua kama ni chaguo sahihi au ataiporomosha timu hiyo kutoka ilipo sasa ‘TOP 2 VPL’ kwa misimu mi 4 mfululizo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment