Usiku wa May 21 2016 vyombo vingi vya
habari za michezo barani Ulaya vinategemea kuandika stori tofauti na
iliyozoeleka kuhusu tetesi za Jose Mourinho, tetesi zilizopo kwenye headlines kwa muda mrefu ni kuhusu klabu ya Man United kuripotiwa kuwa itampa Jose Mourinho kazi ya kuifundisha klabu yao.
Hiyo ndio habari iliyopo kwenye headlines kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, lakini leo May 21 2016 ndio imeripotiwa na Metro na gazeti la Hispania AS kuwa baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la FA utakaochezwa leo katika uwanja wa Wembley, kati ya Man United dhidi ya Crystal Palace, Man United watamtangaza Mourinho kuwa kocha wao.
Matokeo ya mchezo wa fainali leo May 21 2016 hauwezi kuokoa kibarua cha kocha Louis van Gaal hata kama atafanikiwa kutwaa taji hilo, kwani uongozi wa Man United haujafurahishwa na Man United kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment