Burt Kwouk ambaye alijulikana sana kwa kuigiza kama Inspekta Clouseas manservant Cato katika filamu za Pink Panther amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Alishiriki katika filamu kadhaa za Pink Panther mkabala na Peter Sellers kama mfanyikazi wa Clouseas ambaye kila mara alimshambulia mwajiri wake ili kumuweka tayari kwa jambo lolote.
Pia alikuwa nyota wa kipindi cha BBC sitcom Last of the Summer Wine kutoka 2002 hadi 2010.
Akiwa mzaliwa wa Manchester ,lakini akililewa mjini Shanghai, nyota huyo alituzwa tuzo la OBE mwaka 2011 mjini New York.
Taarifa iliotolewa na ajenti wake ilisema: Mwigizaji Burt Kwuok amefariki.
Familia yake itakuwa na mkutano wa mazishi yake lakini kutakuwa na hafla ya kumkumbuka siku ya baadaye.
Kwuok pia aliigiza katika filamu za James Bond ikiwemo Goldfinger na You Only live Twice.
No comments:
Post a Comment