Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos leo Jumatatu ya May 30 2016, amenukuliwa na vyombo vya habari hususani dailymail akithibitisha kuwa katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake dhidi ya timu ya Uingereza utakaochezwa June 2 2016 katika uwanja wa Wembley Cristiano Ronaldo na Pepe hawatocheza.
Fernando Santos amesema hayo kutokana na nyota hao kuwa na uchovu, kwani toka wamalize mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu yao ya Real Madriddhidi ya Atletico Madrid uliochezwa May 28 2016 Milan Italia, hawajapata muda wa kupumzika hivyo wanahitaji wiki moja ya kupumzika.
“Siwapumzishi kwa sababu ya kukwepa majeruhi ila ni kwa ajili ya kuwaweka fiti tu, nafikiri Cristiano Ronaldo atajiunga na timu Jumamosi akiwa na hali ya kujiamini, ni mchezaji bora wa dunia na yeye ni muhimu kwa timu”
No comments:
Post a Comment