Mdororo katika uchumi wa Uchina na vilevile hali ngumu ya kiuchumi duniani ni jambo ambalo limepelekea nchi nyingi za bara la Afrika kukabiliwa na nakisi ya bejeti. Afrika Kusini ambayo inahesabiwa kuwa moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika pia inakabiliwa na hali ngumu ya uchumi ambapo uchumi wake unatathminiwa kukuwa kwa asilimia ndogo sana mwaka huu. Mivutano ya kisiasa na upinzani dhidi ya Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo ni jambo ambalo linashirikiana na ukame na vilevile kupungua thamani ya sarafu ya taifa katika kupunguza ustawi wa uchumi wa nchi hiyo. Mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na Elnino yamevuruga pakubwa sekta za kilimo katika nchi za mashariki na kusini mwa bara la Afrika, zikiwemo za Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe na Malawi. Kupungua kwa mazao ya kilimo nchini Zimbabwe na bei ya shaba katika soko la kimataifa ni masuala muhimu ambayo yameathiri uchumi wa nchi hiyo na Zambia ambayo huzalisha kiwango kikubwa cha shaba duniani. Katika eneo la mashariki mwa Afrika ukame umeathiri sana Ethiopia kwa kiwango ambacho kilikuwa hakijawahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa iliyopita. Ni kwa kuzingatia suala hilo ndipo wataalamu wa IMF wakatabiri kwamba uchumi wa nchi hiyo utapungua kutoka asilimia 10 mwaka uliopita hadi asilimia 4.5 mwaka huu.
Friday, May 13, 2016
Jukwaa la kimataifa la uchumi kwa ajili ya Afrika lafanyika Rwanda

Unknown
Web Developer
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment