Monday, March 28, 2016

Rouhani na Putin: Wasyria watajiamulia mambo yao



Rouhani na Putin: Wasyria watajiamulia mambo yao
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia juu ya udharura wa wananchi wa Syria kuachiwa wajiamulie mambo yao wenyewe.
Rais wa Iran amesisitiza kama ninavyomnukuu: Wananchi wa Syria tu ndio wanaoweza kujichukulia maamuzi kuhusiana na mustakbali wa mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo." Mwisho wa kunukuu.
Rais Rouhani amesisitiza juu ya udharura wa kudumishwa usitishaji vita na kwamba, mazungumzo ya kisiasa kuhusu mgogoro wa Syria yanapaswa kuongeza kasi. Aidha amebainisha kuwa, usitishaji vita huo na mazungumzo ya amani ya Syria ni mambo ambayo hayapaswi kutia dosari katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Syria.
Rais wa Iran ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio ya hivi karibuni ya jeshi la Syria ya kukomboa miji kadhaa ya nchi hiyo na kubainisha kuwa, mafanikio hayo yanaonesha uwezo wa jeshi la nchi hiyo.
Kuhusiana na uhusiano wa Tehran na Moscow, Rais Rouhani amesema katika mazungumzo hayo na Rais Vladimir Putin kwamba, Iran inakaribisha kwa mikono miwili ustawishaji wa uhusiano kati yake na Russia.
Kwa upande wake Rais Vladimir Putin amesisitiza juu ya udharura wa kutekelezwa hatua kali za kiulinzi na kiusalama katika mipaka ya Syria kwa shabaha ya kuzuia upenyaji wa magaidi na kuingizwa silaha.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment