Sunday, March 20, 2016

14 wauawa kwenye ajali Uhispania



Image captionBasi hilo lilikuwa likisafirisha wanafunzi wa kigeni.
Takriban watu 14 wameuawa wakati basi moja lililokuwa likisafirisha wanafunzi wa kigeni kuhusika kwenye ajali ya barabarani katika barabara kuu nchini Uhuspania kati ya miji ya Barcelona na Valencia.
Wengi kati ya watu 57 waliokuwa ndani ya basi hilo walikuwa ni wanafunzi waliohudhuria mpango unaojulikana kama Erasmus, na walikuwa wakirejea kutoka Barcelona baada ya kuhudhuria warsha ya kufyatua fataki.
Image captionDereva wa basi alinusurika na amepelekwa kituo cha polisi
Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la Freginals kilomita 150 kusini mwa Barcelona. Uraia wa wale waliuawa na 43 waliojeruhiwa haujathibitishwa wala kile kilichosabisha ajali hiyo.
Waziri wa masuala ya ndani wa eneo la Catalonia Jordi Jane alisema kuwa dereva wa basi aligonga kifaa upande wa kulia ambapo basi likaelekea upande wa kushoto na kisha kugonga gari llilokuwa likitokea upande mwingine.
Dereva wa basi hilo alinusurika ajali hiyo na amepelekwa katika kituo cha polisi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment