Wednesday, May 11, 2016

Justin Bieber: Sitapiga picha na mashabiki



Image captionJustin Bieber asema hatopiga picha tena na mashabiki wake
Iwapo hujagundua basi ujue kwamba nyota wa muziki wa Pop Justin Bieber yuko katika ziara ya ulimwengu.
Kwa sasa yuko nchini Marekani ambapo alionekana amepumzika katika mbuga moja kabla ya tamasha yake mjini Boston.
Image captionBieber alivyoandika katika mtandao wa instagram
Bieber ambaye alikuwa hana viatu aliwavutia mashabiki lakini akakataa kuzungumza nao hadi watakapoweka simu zao chini.
Haijulikani iwapo picha alizochukua na mashabiki wake katika lango la mbuga hiyo zilikuwa za mwisho,lakini baadaye jioni alichapisha katika mtandao wake wa Instagram kwamba hatapiga picha tena na mashabiki.
Image captionHivi ndivyo mashabiki wake walivyomjibu
''Iwapo utakutana nami mahali ujue kwamba sitapiga picha tena'',aliandika.
Alielezea vile watu hawaezi hata kumsalimia ama kujua kwamba hata yeye ni binaadamu na hivyobasi kumfanya kujihisi kama mnyama na sasa anataka kuheshimiwa.
Image copyrightTWITTER
Image captionJustin Bieber aiwa nchini Marekani
Aliongezea: Najua kwamba watu hawatafurahia lakini hakuna mtu anayenidai picha.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment