Wednesday, March 23, 2016

Watatu wa ajali ya Bagamoyo wazikwa



MIILI ya watu watatu kati ya sita waliokufa katika ajali ya gari iliyotokea kwenye msafara wa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Suleiman Jaffo na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, imezikwa.
Watu hao ambao ni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mkoa wa Pwani, walifariki juzi baada ya kupata ajali katika eneo la Kerege, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Mary Kisimbo alisema, tayari kuna marehemu ambao wameshazikwa huku wengine wakisubiri kusafirishwa baada ya taratibu kukamilika. Aliwataja ambao wameshazikwa kuwa ni dereva wa Tasaf Makame Ally ambaye alizikwa juzi na dereva wa Mkurugenzi Khalid Hassan aliyezikwa jana.
Alisema mwili wa Mkuu wa Idara ya Mipango ba Uchumi, Hilda Msele unatarajiwa kusafirishwa kwenda kwao mkoani Morogoro ambapo maziko yake yatafanyika leo, wakati Mwanasheria wa wilaya Tunsiime Duncan na Mchumi Ludovick Pallangyo wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Arumeru na Marangu kwa ajili ya mazishi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment