Monday, March 28, 2016

Sisitizo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran la kuimarishwa uwezo wa makombora wa Tehran



Sisitizo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran la kuimarishwa uwezo wa makombora wa Tehran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema kuwa, hatua za Marekani kuhusu mpango wa makombora ya nchi hii, zinatakiwa kujibiwa haraka na uwezo wake wa makombora.
Zarif ambaye alifuatana na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan, aliyasema hayo Jumamosi ya juzi mjini Islamabad, mji mkuu wa nchi hiyo katika radiamali yake kufuatia vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya sekta ya makombora ya Iran. Katika radiamali hiyo, waziri Zarif amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa zaidi uwezo wa makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema, Tehran haijiwekei mipaka yoyote katika sekta yake ya makombora na kusema kuwa, mipango hiyo ya makombora haina mahusiano yoyote na silaha za nyuklia. Wakati huo huo mkuu wa idara ya udiplomasia nchini Iran amesema kuwa, kwa mujibu wa amri na sisitizo la rais kwa Waziri wa Ulinzi, uwezo wa makombora wa Iran utaimarishwa zaidi. Duru za kisiasa na habari za Magharibi zilikuwa zimedai kuwa, mpango wa makombora ya balestiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni tishio kwa eneo hususan kwa waitifaki wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. Viongozi wa Washington wanadai kuwa, ili kukabiliana na makombora hayo ya balestiki ya taifa hili, kuna udharura wa kuwekwa ngao za makombora kupitia kuimarisha uwezo wa silaha wa nchi za Kiarabu wanachama wa Baraza la Ghuba ya Uajemi. Hapana shaka kwamba, matamshi hayo yanapitia harakati zenye lengo la kuboresha soko la mauzo ya silaha kwa nchi hizo za Kiarabu za ukanda wa Ghuba ya Uajemi, ambazo ni waitifaki wakubwa wa Marekani katika eneo hili. Takwimu zinaonyesha kwamba, wale ambao wamekuwa wakitoa makelele ya propaganda kufuatia maonyesho ya makombora ya Iran, waliziuzia nchi za eneo la Mashariki ya Kati silaha zenye thamani ya zaidi ya Dola bilioni 100 za Kimarekani. Sisitizo la viongozi wa White House juu ya udharura wa kushadidishwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia vitisho hewa vya istilahi ya kile kinachosemwa kuwa ni uwezo wa makombora wa Iran, linaenda sambamba pia na hatua za kampeni za kuendelezwa vikwazo vingine visivyohusiana kabisa na masuala ya nyuklia. Katika fremu hiyo, Wizara ya Hazina ya Marekani Alkhamisi iliyopita iliyawekea vikwazo mashirika sita ya Iran na wafanyabiashara wawili wa Uingereza kwa tuhuma za kushirikiana na shirika la ndege la Mahan na pia uwezo wa makombora wa Iran. Hatua hizo zimechukuliwa katika hali ambayo, siasa za kiulinzi za Tehran daima zimekuwa zikifanyika kupitia mikataba ya kimataifa na kamwe hazikinzani na makubaliano ya nyuklia. Hata majaribio ya makombora ya Iran nayo yanafanyika ndani ya fremu hiyo hiyo. Swali la msingi hapa ni kwamba, je ni kwa nini makombora ya Iran yazushe makekelele yanayofanywa kupitia kampeni za kueneza chuki dhidi ya Iran na kuyafanya mataifa mengine duniani yaogope kushirikiana na Iran ilhali makombora hayo yapo kwa ajili tu ya kujilinda nchi hii mbele ya vitisho vya adui na wala hayaendi kinyume na sheria za kimataifa? Ukweli ni kwamba, hakuna nchi yoyote yenye haki za kuizuia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kujiimarisha kimakombora. Hivyo sisitizo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran la kuimarishwa uwezo wa makombora wa Tehran, limetolewa katika fremu hiyo hiyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment