Peter Okoye wa Psqaure amemaliza tofauti zake na kituo cha runinga cha Sound City baada ya kituo icho kuacha kupiga nyimbo za kundi hilo tangu mwaka 2014.
Tofauti za wasanii wa kundi la Psquare na kituo icho zilianza baada ya wasanii hao kukataa kuperform kwenye tamasha la kituo icho kwa kutofautiana na kwenye makubaliano ya malipo ndipo kituo kikaacha kupiga kazi za wasanii wa kundi hilo kwa madai ya kudhalauliwa.
Hata hivyo, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Peter Okoye amemaliza tofauti zake na Sound city siku chache baada ya kutofautiana mwanamuziki mwenzake wa kundi hilo kuhusiana na kubadilisha uongozi wao, Peter ameandika “Thank you @soundcityafrica @soundcitytv @tajadepetu and all the entire team! Remain blessed always.”
Taarifa hizi zimekuja siku chache baada ya Peter kuachia wimbo wa peke yake siku chache zilizopita tangu agombane na mwanakundi mwenzake wa Psquare.
No comments:
Post a Comment