Monday, March 21, 2016

Shein atangazwa mshindi wa urais Zanzibar



12:30 Matokeo kamili ya uchaguzi. Yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.
12:20 Mgombea wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein amekabidhiwa cheti wa ushindi wa urais.
12:08 Dkt Ali Mohammed Shein atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.
11:57 Mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein yumo ukumbini.
11:54 Bw Jecha kwa sasa anatoa hotuba ya kufungua kikao cha kutangazwa kwa matokeo.
11:49 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha amewasili ukumbi wa kutangaziwa matokeo. Tume imesema itatangaza matokeo yote muda mfupi ujao.
11:27 Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein aongoza matokeo ya awali ya urais majimbo ya Chonga kura 3598, Ziwani (2890), Wawi (4147), Ole (3818), Chake Chake (4551). Matokeo rasmi bado yanasubiriwa.
11:00 Baadhi ya waliowania urais wamefika ukumbini na kuketi. Mmoja wao ni mgombea wa ADC Hamad Rashid.
10:30 Wanahabari, waangalizi na maafisa wengine wa uchaguzi tayari wamo ukumbini wakisubiri kuanza kutangazwa kwa matokeo.
10:20 Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:
1Khamis Iddi LilaACT-W
2Juma Ali KhatibADA-TADEA
3Hamad Rashid MohamedADC
4Said Soud SaidAFP
5Ali Khatib AliCCK
6Ali Mohamed SheinCCM
7Mohammed Massoud RashidCHAUMMA
8Seif Sharif HamadCUF
9Taibu Mussa JumaDM
10Abdalla Kombo KhamisDP
11Kassim Bakar AlyJAHAZI
12Seif Ali IddiNRA
13Issa Mohammed ZongaSAU
14Hafidh Hassan SuleimanTLP
10:15 Ulinzi mkali umewekwa katika ukumbi wa kutangazia matokeo. Mbwa wa ulinzi pia wametumika kukagua eneo hilo, ambalo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Selim Jecha Selim anatarajiwa kutumia kutangaza matokeo.
10:00 (Saa za Afrika Mashariki). Hujambo! Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar Jumapili yanatarajiwa kutangazwa leo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu kutangazwa kwa matokeo hayo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment