Wednesday, March 23, 2016

Serikali yakiri kuna changamoto sekta ya madini


WIZARA ya Nishati na Madini imesema pamoja na kwamba zipo changamoto mbalimbali katika sekta ya madini, lakini changamoto hizo si kigezo cha sekta hiyo kuitwa jipu au tezi, kama ilivyoelezwa na Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Ami Mpungwe.
Aidha, imesema Serikali ya Awamu ya Tano itachukua hatua kali zaidi kwa watu wote wanaofanya biashara ya Tanzanite kwa magendo ili madini hayo yailetee faida nchi ikiwemo ajira kwa wananchi na kukuza mapato.
Hayo yalisemwa katika taarifa ya wizara hiyo iliyokuwa inatoa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini kuwa zaidi ya jipu, tuhuma zinazodaiwa kutolewa na Balozi Mpungwe na kunukuliwa na gazeti moja la kila siku la Kiswahili (si HabariLeo), katika toleo lake la Machi 20, mwaka huu.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Profesa James Mdoe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Madini, imesema pamoja na kuwepo kwa changamoto, ipo tayari kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuondoa changamoto katika sekta ya madini.
Ilisema kuwa Balozi Mpungwe amekuwa mdau mkubwa wa sekta ya madini kwa muda mrefu hasa katika uchimbaji madini ya Tanzanite katika Kitalu C, Mirerani wilayani Simanjiro katika Mkoa wa Manyara.
“Mwaka 2000, kitalu hiki kilikuwa na leseni maalumu ya uchimbaji tanzanite iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mirerani Mining Limited (MML) huku Balozi Mpungwe akiwa ni Mjumbe wa Bodi ya kampuni hiyo,” ilieleza taarifa na kuongeza kuwa mwaka 2000, kampuni hiyo ilibadilishwa jina na kuwa African Gem Resources (AFGEM) na Aprili 2004 jina likabadilika na kuwa TanzaniteOne Mining Limited.
Ilisema Januari 2015, TanzaniteOne iliuzwa kwa kampuni ya Sky Associates na mnamo Juni 2015, Sky Associates iliingia ubia na serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa hisa 50 kwa 50.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, inashangaza kwamba baada ya Kampuni ya TanzaniteOne ambayo Balozi Mpungwe amekuwa na hisa kwa muda mrefu, kuuzwa kwa Sky Associates anadai sekta ya madini ni zaidi ya jipu, ni tezi.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment