Friday, March 11, 2016

Paul Scholes:Manchester United haifai



Image captionWachezaji wa Manchester United
Manchester United ilikuwa haifai na haikuwa na mpangilio wowote ilipofungwa 2-0 na Liverpool kulingana na Paul Scholes ambaye alikuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Paul Scholes.
Daniel Sturridge na Firmino walifunga bao kila mmoja na kudidimiza matumaini ya Manchester United huku David De gea akizuia mashambulio mengi ya Liverpool.
Scholes ambaye aliichezea Manchester United mara 718 aliambia BT Sport kwamba kilabu hiyo ya Old Trafford huwa na viwango fulani lakini kufikia sasa imefeli kuafikia viwango hivyo.
Aliongezea:Liverpool ilikuwa na mpango wa kucheza,Lakini United hawakuwa na mpango wowote.
Image copyrightReuters
Image captionMkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp
Awamu ya pili ya mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa Old Trafford Alhamisi ijayo.
''Manchester United inafaa kuwania ligi ya Uingereza na kombe la vilabu bingwa'',alisema Scholes.
Wametumia pauni milioni 300 na bado wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi.
Image copyrightPA
Image captionPaul Scholes
Wameshushwa hadi katika ligi ya Europa baada ya kushindwa katika kombe la vilabu bingwa.
Wanafaa kushindana na Barcelona,Real Madrid na Bayern.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment