Monday, March 28, 2016

Mufti wa Syria: Tuliitahadharisha Ulaya kuhusu hatari ya ugaidi



Mufti wa Syria: Tuliitahadharisha Ulaya kuhusu hatari ya ugaidi
Mufti Mkuu wa Syria Sheikh Ahmad Badruddin Hassoun amesema nchi hiyo ilikwisha zitahadharisha hapo kabla nchi za Ulaya kuhusu hatari ya kupenya na kuenea ugaidi katika nchi hizo.
Sheikh Hassoun ameyasema hayo katika mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa Ufaransa unaoitembelea nchi hiyo na kuongeza kuwa Syria imepigana vita na ugaidi na misimamo ya kufurutu ada kwa niaba ya Ulaya na kuzilinda nchi za bara hilo.
Mufti Mkuu wa Syria amesisitiza kuwa sambamba na kupambana na ugaidi nchi hiyo imefanya ya jitihada pia za kufanikisha mapatano na maridhiano ya kitaifa.
Sheikh Ahmad Badreddin Hassoun aidha ametaka baadhi ya nchi ikiwemo Uturuki, Saudia na Qatar ziache kuunga mkono magaidi na pia ziache kuingilia masuala ya ndani ya Syria.
Katika mazungumzo aliyofanya na wabunge wa Bunge la Ufaransa hapo jana, Rais Bashar al-Assad wa Syria alisema safari ya ujumbe huo nchini Syria na kupata taarifa za ukweli halisi ulivyo katika maeneo na miji mbalimbali ya nchi hiyo kunaweza kusaidia kurekebisha siasa na sera ghalati za baadhi ya nchi ikiwemo Ufaransa kuhusiana na matukio ya Syria.
Safari ya wabunge wa Ufaransa ni ya nne kufanywa na ujumbe wa bunge la nchi hiyo huko nchini Syria katika miezi ya hivi karibuni.../
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment