Saturday, March 19, 2016

Mshukiwa mkuu wa shambulio la Paris akamatwa



Image copyrightEVN
Image captionMaafisa wa polisi nchini Ubelgiji wakimkamata mshukiwa
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameonya kuwa mitandao ya kigaidi barani Ulaya inaendelea kuimarika licha ya kukamatwa kwa mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris.
Salah Abdeslam alikamatwa wakati wa uvamizi uliofanywa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Ubelgiji katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels baada ya kupigwa risasi kwenye mguu.
Image copyright
Image captionEneo lililovamiwa na maafis wa polisi
Mtu mwingine ambaye pia anashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi hayo ya mwezi Novemba alijeruhiwa na kukamatwa na kwa ujumla watu watano walikamatwa.
Image copyrightReuters
Image captionMaafisa wa polisi
Bwana Hollande alisema kuwa vita havitakwisha hadi kila mmoja aliyehusika kwenye shambulizi la Paris akamatwe. Watu 130 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment