Monday, March 28, 2016

Marekani na kuendelezwa propaganda chafu dhidi ya Iran



Marekani na kuendelezwa propaganda chafu dhidi ya Iran
Gazeti la al Sharqul Ausat linalochapishwa mjini London, Uingereza limechapisha ripoti mbili katika toleo lake jipya likinukuu hukumu iliyotolewa na mahakama moja ya New York nchini Marekani dhidi ya Iran kuhusu faili la mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Gazeti hilo linalomilikiwa na Wasaudia limeandika kuwa, jaji wa mahakama hiyo ya New York ameihukumu Tehran kulipa faini ya dola bilioni 10.7 ambazo zinaambatanishwa na asilimia 9 ya fedha hizo kama riba ya kabla ya kutolewa hukumu hiyo na kufikia dola bilioni 21. Hukumu hiyo kwa hakika imetegemea ushahidi wa uongo uliotolewa na maafisa wawili wa shirika la ujasusi la Marekani CIA.
Ripoti ya gazeti la al Sharqul Ausat imeashiria kuwa kwa mujibu wa yaliyosemwa mahakamani hapo imedaiwa kuwa Iran ililisaidia kwa fedha kundi la al Qaida ili liweze kutekeleza mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Katika mchezo huo wa kubuni, matukio yote ya kigaidi yaliyotokea katika miaka iliyopita yamehusishwa na Iran na harakati ya Hizbullah, na bila ya kuwa na ushahidi wowote imedaiwa kuwa "ushirikiano wa al Qaida na Iran kwa upande mmoja na ushirikano wake na Hizbullah katika upande mwingine haukuishia katika kupanga mashambulizi ya Septemba 11 pekee".
Katika mchezo huo wa mahakama hiyo ya kimaonyesho imedaiwa kwamba Iran ilihusika pia na mlipuko wa minara ya al Khubar nchini Saudi Arabia hapo mwaka 1998, mashambulizi yaliyolenga balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1996 na mlipuko ulioilenga manowari ya kivita ya Marekani ya USS Cool katika pwani ya Yemen mwaka 2000.
Ripoti ya al Sharqul Ausat imedai kuwa, watu waliowasilisha mashtaka mahakamani walikuwa na ushaidi uliosema kuwa, Iran ililisaidia kifedha kundi la kigaidi la al Qaida.
Madai hayo yametolewa wakati dunia nzima inajua kwamba, idadi kubwa ya watu wanaoshiriki katika mashambulizi ya kigaidi likiwemo lile la Septemba 11 huko Marekani na wale walioko katika makundi kama al Qaida na Jabhatul Nusra ni raia wa Saudi Arabia au ni watu waliotayarishwa na kupikwa na Marekani yenyewe. Hata hivyo jaji wa mahakama ya New York amechukua uamuzi wa kuiondoa Saudi Rabia katika kesi hiyo.
Wakati huo huo waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, amekiri kwamba Marekani ilihusika katika kuunda na kuanzisha makundi ya Qaida na Daesh. Kwa mfano tu Clinton amekiri waziwazi katika kitabu chake alichokipa jina la "Hard Choices" au Machaguo Magumu, kwamba Marekani ilihusika katika kuanzisha kundi la Daesh.
Marekani pia inayaunga mkono makundi ya kigaidi likiwemo kundi la MKO na imekuwa ikiyatumia kwa ajili ya kufikia malengo yake. Katika Upande mwingine Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni miongoni mwa wahanga wa mashambulizi na harakati za makundi hayo ya kigaidi yanayosaidiwa na kuungwa mkono na Marekani.
Kwa kutilia maanani hayo yote ni kichekesho kuituhumu Iran kuwa inahusika na matukio ya kigaidi. Madai kama hayo na kutolewa hukumu kama hizo kupitia mahakama za kimaonyesho tu za Marekani ni mbinu inayotumiwa kwa miaka sasa kwa ajili ya kutwaa mali za Iran na kudumisha uhasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Kuanzishwa kwa mahakama kama hizo eti zinazoshughulikia mashtaka yaliyowasilishwa na watu binafsi dhidi ya Iran kwa hakika ni mbinu tu inayotumiwa na Marekani kwa ajili ya kudumisha siasa na sera za uhasama na uadui wake na vilevile kuchafua jina na sura ya Iran.
Madai ya Washington kuhusu miradi ya kuzalisha makombora nchini Iran na kutolewa maazimio ya kisiasa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran pia vinaweza kutathminiwa katika mkondo huo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment