Friday, March 18, 2016

Man Utd na Liverpool washtakiwa na Uefa



mashabikiImage copyrightRex Features
Image captionMashabiki walikabiliana wakati wa mechi
Klabu za Manchester United na Liverpool zimeshtakiwa na Uefa kufuatia fujo za mashabiki wakati wa mechi ya marudiano ya Europa League iliyochezwa Alhamisi.
Klabu hizo zilitoka sare 1-1 mechi hiyo ya marudiano ya hatua ya 16 bora iliyochezewa uwanja wa Old Trafford.
Mashabiki wa timu zote mbili walionekana wakikabiliana uwanjani na viti vilirushwa na mienge kuwashwa wakati wa mechi hiyo.
Watu watano walikamatwa.
Klabu zote mbili zimeshtakiwa na makosa ya mashabiki kuzua fujo pamoja na vitu kurushwa uwanjani.
Manchester United pia wanatuhumiwa kufunga ngazi nao Liverpool wanatuhumiwa kuchelewesha mechi, mashabiki kurusha matusi na kuwasha mienge.
UtdImage copyrightReuters
Image captionManchester United waliondolewa kwa matokeo ya jumla
Liverpool walisonga kwa jumla ya mabao 3-1 kutokana na ushindi wao wa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza.
Kesi hiyo itasikizwa na bodi ya nidhamu ya Uefa mnamo 19 Mei, siku ambayo fainali ya Europa League itakuwa ikichezwa mjini Basel.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment