Michezo ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON ambayo itapigwa juma hili na juma lijalo ili kuzipata timu zitakazo shiriki michuano hiyo itakayofanyika Gabon mwanzoni mwa mwaka ujao. Presha imeanza kuongezeka kabla ya mechi za mwisho za makundi kuchezwa mwezi June na September.
Shaffihdauda.co.tz inakupa fursa ya kutupia jicho la tatu vitu vitano kwenye soka la Afrika wiki hii…
Siasia na Nigeria yake atatoboa?
Kwenye Group G, Nigeria itakuwa mwenyeji wa Misri siku Ijumaa kabla ya kusafiri hadi Cairo kwenye mechi ya marudiano siku nne baadaye. The Super Eagles wako nyuma ya wapinzani wao hao kwa pointi mbili na watahitaji kushinda japo mchezo wao mmoja kati ya mechi hizo ili waweze kuwa kwenye mazingira ya kuongoza kundi.
Timu 13 zitakazoongoza makundi yao zitafuzu moja kwa moja na zile timu mbili ambazo zitamaliza nafasi ya pili zikiwa na matokeo bora. The Super Eagles wako kwenye presha ya hali ya juu kuhakikisha wanapata matokeo.
Kocha wa muda Samson Siasia atamkosa beki wake Kenneth Omeruo na kunauwezekano pia wa kumkosa Leon Balogun ambaye klabu yake imesema imemuweka pembeni kutokana na kuuguza jeraha.
Hata hivyo kocha huyo anawachezaji wengi wa kimataifa wenye uzoefu wa hali ya juu kuanzia Odeon Ighalo, Alex Iwobi, Victor Moses pamoja na John Obi Mikel wanaofanya vyema kwenye English Premier League.
Kwa upande wa kocha mpya wa Misri Hector Cuper, yeye anaonekana kujiamini akisema kwamba: “Mara zote huwa siahidi chochote kitakachotokea, lakini naamini tunaweza kuwashinda Nigeria”.
Afrika Kusini watazuia kutupwa nje ya mashindano?
Hali ya Bafanabafana inaonekana ni mbaya kuelekea mchezo wao dhidi ya Cameroon kuliko ile ya Nigeria. Mabingwa hao wa mwaka 1996 wako mkiani mwa Group M wakiwa na pointi moja pekee pointi tano nyuma ya vinara na watakuwa ugenini kucheza dhidi ya wapinzani wao ‘Indomitable Lions’ siku ya Jumamosi.
Kocha mpya wa Cameroon Hugo Broos ambaye hakuwepo wakati kikosi hicho kikipata pointi sita amemjumuisha kwenye kikosi Alexandre Song ambaye hajaitwa kwenye timu hiyo tangu imu hiyo iliposhiriki michuano ya kombe la dunia 2014, Brazil.
Lakini kocha huyo ameingia kwenye sintofahamu baada ya kumpiga chini kiungo wa Shalke Joel Matip lakini amemjumuisha kaka yake Mavin anayekipiga kwenye Bundesliga na klabu ya Ingolstadt.
“Ninaimani Joel hakuwa na ari na kutaka kuja”, kocha huyo aliviambia vyombo vya habari vya Ujerumani. “Nahitaji wachezaji wenye morali ya kuwa sehemu ya kikosi na kama si hivyo basi bora wakae nyumbani”.
Mbelgiji huo atamkosa pia striker wa Porto Vincent Aboubakar kwenye mchezo wa kwanza kutokana na kutumikia adhabu. Kocha wa Bafanabafana Shakes Mashaba ameita kikosi cha wachezaji wenye uzoefu lakini kukiwa na wachezaji ambao walioitwa kwa mara ya kwanza. Anatambua kupoteza mchezo huo kutaifanya timu yake itupwe nje ya michuano wiki hii, “mechi hii ni lazima tushinde, ukiangalia msimamo wa kundi unatuambia tunahitaji kushinda nyumbani na ugenini”.
Samaki wakubwa watawala wadogo?
Morocco wakiwa chini ya kocha mpya Herve Renard, na Cape Verde vinara wa Group F wakiwa na pointi sita watakutana uso kwa uso na The Blue Sharks ambao wako vizuri kwa sasa wakijivunia wastani wao mzuri wa magoli. Mabingwa watetezi Cote d’Ivoire katika hali ya kushangaza wamejikuta wako nafasi ya pili nyuma ya Sudan kwenye Group . Hata hivyo, wakiwa kwenye kundi lenye timu tatu, wameshacheza mchezo mmoja pekee na kutoka sare kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Sierra Leone. Tembo hao wtacheza dhudi ya Sudan na kama wanataka kuongoza kundi hilo, wanatakiwa wasipoteze michezo yao.
Kocha Michel Dussuyer hajaacha kitu na amemshawishi Yaya Toure kurejea kwenye timu. Mchezaji huyo bora wa zamani wa Afrika anaunda kikosi chenye nyota wenye uzoefu kama Solomon Kalou, Serey Die, Wilfred Bonny na Max Gradel. Congo na Zambia zitakutana kwenye michezo ya Group E wakati Algeria ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuongoza Group J itacheza dhidi ya Ethiopia.
Timu zisizotarajiwa zinaweza kuishangaza Afrika
Kwenye kundi A, Liberia inaweza kuendelea kuongoza kundi kwa ushindi wa pili wiki hii dhidi ya Djibout. Wakiwa wameichapa Tunisia September mwaka jana, timu iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda. The Lone Stars wanajaribu kuifukuzia Togo kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya tatu. Sudan Kusini wakiwa wamepata ushindi kwa mara ya kwanza kwenye mbio za kuwania kufuzu michuano ya AFCON walipoiunga Equatorial Guinea, wanatarajia kuendelea na safari yao watakapocheza dhidi ya Benini kwenye mechi za Group C.
Kibonde mmoja anaweza kusimama
Mechi ya kuvutia katika Group l itakuwa ni kati ya Zimbabwe na Swaziland ambazo zitakutana mara mbili wiki hii. Zimbabwe tarari imewahi kufuzu mara mbili kwenye fainali za michuano ya Afrika wakati Swaziland bado haijawahi kufanya hivyo hata mara moja kwenye soka la Afrika. Sare au ushindi utaishuhudia timu moja ikikaa kwenye mzingira mazuri ya kufuzu kucheza fainali hizo, timu zote zinapointi nne zikiwa zinaongoza kundi juu ya Malawi na Guinea.
No comments:
Post a Comment