Thursday, March 17, 2016

Mahakama yasimamisha uteuzi wa Lula Brazil



Image copyrightAFP
Image captionAliyekuwa rais wa Brazil Luiz Lula da Silva
Mahakama moja nchini Brazil imesimamisha uteuzi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Luiz Inacio Lula da Silva kama mkuu wa utumishi wa uma na mrithi wake Dilam Rousseff.
Agizo hilo la mahakama mjini Brasilia linajiri mda mfupi baada ya Lula kuapishwa katika wadhfa huo.
Mapema ,wafuasi wake na wale wanaompinga walifanya maandamano nje ya jumba la rais.
Wakosoaji wa Lula wanamtuhumu kwa kuchukua wadhfa huo ili kukwepa mashtaka ya ufisadi yanayomkabili.
Kulikuwa na maandamano katika miji kadhaa ya Brazil usiku kucha.Rais Rousseff anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi kufuatia madai ya kutoa hongo yanayhusishwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Petrobras.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment