Friday, March 25, 2016

LAAC wakataa taarifa ya Kigoma Ujiji.





KAMATI za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) imekataa kupokea taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri ya Kigoma Ujiji kwa kuwa haioneshi picha halisi ya halmashauri hiyo.
Aidha, imesema kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha katika halmashauri hiyo na ukiukwaji wa taratibu katika matumizi ya fedha za Serikali ambapo imeonesha kuna fedha zimetolewa bila maelezo yanayoeleweka.
Akitoa maagizo hayo katika LAAC jana, Makamu Mwenyekiti wake, Abdallah Chikota ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nanyamba alisema haikuridhishwa na majibu yaliyotolewa na viongozi wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji.
“Kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha za halmashauri yenu tunaagiza halmashauri ichukue hatua kwa watumishi wote waliohusika katika ubadhirifu huo na Tamisemi isimamie hili,” alisema Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment