Friday, March 11, 2016

DC Paul Makonda Awapa Wiki Mbili Watendaji wa Kinondoni Kuhakikisha Mashimo Yote Yaliyopo Barabarani Yanazibwa




MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alifanya ziara ya kukagua barabara ya Mwanayama 'A' hadi Makumbusho ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza baada ya kukagua barabara hizo alisema amewapa watendaji wa manispaa ya Kinondoni wiki mbili kushughulikia tatizo hilo kutokana na adha ya magari yanayotumia barabara hiyo.

"Sasa nimeiagiza Manispaa, nimewapa wiki mbili kuhakikisha mashimo yote yawe yamezibwa, na wakishindwa nitawasaidia kuwawajibisha na kuchukua hatua stahiki." Alisema Paul Makonda

Alisema kuwa kuharibika kwa barabara nyingi katika manispaa hiyo ni kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

Makonda alisema fedha zinatolewa kwa ajili ya ujenzi lakini baadhi ya watendaji wanajenga chini ya kiwango na kuwapa adhabu wananchi wanaotumia barabara hiyo.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment