Monday, March 28, 2016

DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI KWA MTINDO WA ‘NYOKA’


DAR ES SALAAM


SHIRIKA la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limebaini wizi mkubwa wa maji kwa mtindo wa ‘nyoka’ kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo.DAWASCO

Akizungumza kwenye operesheni maalumu ya kubaini wizi wa maji, meneja wa Dawasco, Kanda ya Magomeni, Pascal Fumbuka alisema wamebaini wizi huo kufanyika mtaa wa Chama pamoja na Mkundunge iliyopo Sinza na Tandale jijini humo.

Alisema wizi huo wa maji unajulikana kwa jina la wizi wa nyoka ambapo wananchi wamejitengenezea laini za maji kinyemela, kwa kutumia mipira ya kawaida na kutoa maji kutoka umbali mrefu na kuyapitisha kwenye nyumba zao au kuunganisha kwenye ,matenki ya maji na kuuza bila kibali kutoka Dawasco.

Fumbuka alisema wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa laini zote za maji kwa sababu za kiafya, kutoa elimu kwa wakazi hao kuwa hawaruhusiwi kujiunganishia maji, bali wanapaswa kuomba kuunganishiwa na Dawasco.

Alisema hatua nyingine yanayochukua ni kuweka kizimba (kioski) cha maji eneo hilo ili kuwezesha wakazi hao kuendelea kupata huduma ya maji kwa malipo nafuu na kwamba wao wenyewe ndio watakuwa walinzi wa miundombinu hiyo na kuhakikisha bili ya kizimba hicho inalipwa Dawasco.


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment